Kuingizwa kazini kwa Makamu Mkuu wa Chuo

“Nenda kaifanye kazi ya Bwana kwa ukamilifu” Maneno haya yalisemwa na Mkuu wa Chuo kikuu Tumaini Makumira Dr. Alex Malasusa kwa Makamu Mkuu mpya wa Chuo Prof. Faustin mahali. Haya yalifanyika katika hafla ya kumtakia heri Prof. Joseph Parsalaw Makamu Mkuu wa Chuo aliyemaliza muda wake na kumuingiza kazini Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Faustin Mahali.
Tunayo imani kuwa uongozi wake utaimarisha zaidi misingi hiyo na kuleta msukumo mpya katika kufanikisha dira na malengo ya taasisi yetu.Kwa pamoja, tunamkaribisha kwa moyo mkunjufu na tunampa ushirikiano wa dhati katika kutekeleza majukumu yake mapya kwa ufanisi, uadilifu na ubunifu.
Tunamtakia mafanikio mema katika safari hii mpya ya kiuongozi hapa chuoni.