Ujio wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Palamagamba Aidan John Mwaluko Kabudi alikuja kuzuru chuoni kwetu TUMA mnamo tarehe 01/03/2025 kwa lengo la kubariki mchakato wa uanzishaji wa kituo cha Utamaduni na Lugha. Katika hafla hiyo Makamu Mkuu wa Chuo Profesa Faustin Mahali aliishukuru serikali kwa kuona umuhimu wa Lugha ya Kiswahili na kuagiza wizara husika kutilia mkazo uanzishwaji wa vituo hivyo.