Mahafali ya Chuo Kikuu Tumaini Makumira

 

Mkuu wa Chuo Cha Tumaini Makumira(TUMA) ambaye pia ni Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Daktari Alex Geaz Malasusa amewatunuku Astashahada,Stashahada na Shahada mbalimbali kwa wahitimu kutoka fani mbalimbali zinazofundishwa chuoni hapomnamo 30/11/2024.

Katika hotuba yake , Askofu Malasusa aliwapongeza wahadhiri wa chuo kwa juhudi zao katika kuwaandaa wanafunzi vizuri kwa ajili ya kukabiliana na changamoto za ulimwengu wa sasa.