Tumaini Makumira kushiriki maadhimisho ya siku ya wanawake duniani

Watumishi Wanawake kutoka Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira wameshiriki kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani leo Machi 8, 2025 jijini Arusha ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Wanawake ni jeshi kubwa ambalo likiwezeshwa katika masuala mbalimbali nchini huongeza chachu ya utendaji kazi kwa kuzingatia usawa wa kijinsia kwa kushirikiana na wanaume na kuleta maendeleo kwa ustawi wa taifa.
Katika kuadhimisha Siku hiyo, Wanawake wa chuo kikuu Tumaini Makumira walipata fursa ya kushiriki kikamilifu maonesho kuanzia tarehe 01 Machi hadi 08 Machi kwenye Kilele cha Maadhimisho hayo kwa kutoa huduma mbalimbali ikiwa pamoja na kuendelea kukitangaza chuo kikuu cha Tumaini Makumira.
Maadhimisho hayo kwa Mwaka huu yamefanyika Kitaifa Jijini Arusha katika Viwanja vya Sheikh Amri Abeid Karume yaliyobeba kauli mbiu isemayo “Wanawake na Wasichana 2025: Tuimarishe Haki, Usawa na Uwezeshaji”.